Madai 20 ya Lost Genarations: Tunataka yafuatayo kutoka Serikali ya Rais Samia yafanyiwe kazi (2024)

Kwako mheshimiwa Samia Hassan Rais wa Tanzania, Tunahitaji maswala yafuatayo yatatatuliwe kwa faida yetu sote, hii nchi ni ya Watanzania wote, kama kuna kuteseka tuteseke wote na tufurahie maisha wote.

1. Serikali iachane na Uraibu wa Magari ya Kifahari ambayo ni mzigo mkubwa sana kwa walipa kodi. Pesa zinazo tokana na kuacha uraibu wa Magari ya kifahari zielekezwe kusaidia vijana kujiajiri.Serikali inashindana na nanu kwenye anasa? Wanancbi wanataka kuona ahueni za maisha yai, Magari ya Kifahari hayawezi waletea ahueni.

2. Sheria ya kuwalipa mafao Wanawake wa Maraisi wastaafu irudishwe bungeni na ifutwe, Wanawake wa Maraisi wanafadikika na mafao ya Bwana zao, kuwalipa pia na wao ni sawa na double Payments, Pesa hizo bora zielekwezwe kuwanunulia Pedi wasichana wasio kuwa nanuwezo huko vijijini. Tutaomba na sisi Mama zetu walipwe sasa.

3. Serikali iwekeze kwenye mifumo ya kidigitali ili kupunguza pia gharama kuliko ilivyo sasa ambako inakusanya Wakuu wa wilaya au mikoa au Wakurugenzi sehemu moja, kuwahutumua badala ya kutumia njia za kisasa, hii ni matumizi makubwa sana ya pesa za walipa kodi ilihali kuna vijana hawana ajira na kuna Wafanya kazi wana malipo duni sana.Mbona Wazungu huwa tunafanya nao mikutani kidigitali? Serikali inashindwa nini?

4. Viongozi wa Serikali walioko maeneo ambayo sio korofi wapewe magari ya kawaida sana ya kutumia kiliko ilivyo sasa ambako kiongozi kama Mkuu wa wilaya au mkoa pale Dar es salaamu na yeye anapeaa gari linali oaswa kutolewa kwa mkuu wa wilata kule Ngorongori au Handeni, kati kati ya jiji magari ya unjini kubwa ya nini? Wanawinda?

5. Recyciling ya viongozi ifutwe, Kiongozi alikuwa Mbunge kashindwa kura za maoni au kashindwa uchaguzi basi maana yake hafai, kumpatia vyeo tena ni kuwatukana wale walio mktaaa na ni kuwazibia wengine nafasi za wao kulitumikia Taifa. Hakuna watu wenye Copy right ya kulitumikia Taifa. Tuachabe na recycling ya watumishi.

6. Kuondolewe upendeleo wa wazi na mambo ya kujuana kwenye ajira za Serikali, uwazi uwepo na uonekane ukitendeka, ajira zinatolewa sana kwa kujuana, mtu apate ajira kwa uwezo alio nai na sio kwa kujuana na nani. nchi hii ni ya wote sio kikundi fulani.

7. Posho za Wabunge zipinguzwe, wabunge wana aina nyingi sana za posho ilihali watumishi wanao fanya kazi muda mwingi na mazingira magumu kama walimu au watumishi wa afya hawana posho, posho za Wabunge zipunguzwe ziongezewe kwenye posho za kuwalipa watumishi wa hizo Kada.

8. Vikao virefu vya Bunge ni matumizi mabaya ya pesa za umma, Kwa nini wabunge wakae kupitisha bajeti ya kila wizara na pia wake kupitisha jumla ya bajeti yote? Huu mfumo ni mfumo wa upigaji wa pesa za umma. tunataka ubadilishwe. Ni Tanzania pekee bunge hukaaa miezi mitatu na zaidi mfululizo kupitusha bajeti.

9. Tunataka uwazi kwenye mikataba yote inayo ingiwa na Serikali huko nje ya nchi, hii nchi ni ya rai wote milion 60 na zaidi, ilivyo sasa hakuna uwazi wa mikataba na mikataba imejaaa usiri mkubwa sana, ni kitu gani kinafichwa kwenye hii mikataba? tunataka tukijue.

10. Report za CAG zinadharuliwa sana na wanao husika wamekuwa hawachukuliwi hatua zozote, tunaka kujua kwa nini hawachukuliwi hatua? na kuna haja gani kutumia pesa kufanya ukaguzi ambao wahusika wanaachwa kazini wakitamba na wakiendelea kupiga pesa?

11. Uporaji wa aridhi ya wananchi na kuwahamisha maeneo yao ya asili kwa kisingizio cha kupisha wawekezaji ni kuwapora haki zao za kuishi sehemu waitakayo, Kila raia ana idetity yake ana asili yake, hivyo kumuhamisha eneo alilo zaliwa na kukulia na kumwambia akaishi sehemu nyingine ili kupisha wawekezaji ni kinyume na utu,Hii tabia inaota mizizi sasa Tanzania.

12. Serikali itangaze kama Makao makuu ya nchi ni Dodoma au Dar es salaaam, hii ya 50% kwa 50% ni kuwabebesha walipa kodi mzigo kubwa sana, hakuna nchi Duniani yenye ikulu mbili zenye hadhi sawa sawa zaidi ya Tanzania.Ikulu ya Dodoma na Dar es salaam zina hadhi sawa, haya ni matumizi mabay sana ya pesa za walipa kodi wa nchi hii.Ichaguliwe moja.

13. Mazingira ya kodi Tanzania sio rafiki kabisa kwa Watanzania wanao jitafuta kwenye biashara, kodi zimejaa dhuruma, na hazina uhalisia,Kodi zipunguzwe na ziwe ni za uhalisia, na Serikali idhibiti matumizi yake, matumizi ya anasa ya Serikali na rushwa ndio chanzo cha msululu wa kodi.

14. Mazingira magumu ya kuanzisha biashara Tanzania hasa kwa sisi Watanzania tunao jitafuta ni kikwazo, nani anafaidika na mazingira haya magumu? Serikali inafadikika vipi na haya mazingira? Tunataka mazingira rahisi sana ya kuanzisha biashara.

15. Kwa nini Serikali haiwekezi kwenye mifumo ya uwajibikaji? kwa nini ategemewe mtu mmoja yeye ndie awe Police, na hakimu? Tunataka kujua kinachi kwamisha Serikali kuwa na mifumo inara ya uwajibikaji Serikalini.

16.Tunataka mabadiliko kwenye taasisi za umma kwenye utendaji wa kazi, taasisi za umma umejaa uongo mwingi sana, Majivuno na Dharau taasisi za umma haziko kwa ajili ya wanannchi, Mwananchi analazimika kusafiri kutoka Tarime kule Mara kuja Dodoma kupata ufafanuzi wa jambo ambalo angepewa kwa njia ya Simu au Barua pepe, taasisi za umma hazipokei simu, hawajibu barua pepe, tunataka kujua kama wanajiendesha kwa pesa zao au ni hizi hizi za walipa kodi ambao hawawasikilizi na wana wa dharau. Nani pia anafadika na huu mfumo wa hovyo kabisa wa utoaji huduma kwenye taasisi za uuma?

17. Upandaji wa gaharama za maisha ilihali Serikali wao wakiishi kwa anasa, Gharama za Maisha za walipa kodi ziko juu sana, lakini mtaani tunaona jinsi Serikali wao wanavyo ishi maisha ya anasa, hii nchi ni ya wananchi wote milion 60 hivyo sio sawa wengine wataabike na wengine waneemeke kwa jasho la wanao taabika.

18. Ajira ajira ajira ajira, vijana wako mtaani na hawa ndio sasa wanaamua kubadilika na kuwa chawa wa Wanasiasa. Vijana haaana ajira na hakuna mpango wa kuwapatiaa ajira zaidi ya juwataja wajiajir8 wakati huo huo wengine wakijiriwa jwa vimemo tu. Vuingozi wa Serikali hakuna ndugu yao asie kuwa na ajira, wanai taa ika na kuti juwa ba ajira ni wake wasio juana na mtu wa Serikali. Hii sio sawa na pia tujue nani anafadika na hili tatizo ka vijana kuto kuwa na ajira.

19. Serikali inakopa sana lakini haitaki kabisa kudhibiti matumizi ya anasa, na upigaji, Mikopo mingi inaishia mif*ckoni mwa watu na mwisho wa siku ni rai ndio walipaji wa hio mikopo. Serikali kama ilivyo na uraibu wa magari ya anasa pia ina uraibu wa kukopa ila haitaki kuwa na uraibu wa kupambana na wala rushwa.

20. Mikopo ya wanafunzi wa vyuo vikuu inagaliwe, wanafunzi wapewe mikopo asilimia 100 na wakimaliza wapeni ajira warudishe mikopo. Kama pesa ni kikwazi, punguza matumizi ya anasa, Magari, ziara yingi za viongozi hata ndani ya nchi hazina tija, punguza upigaji wa pesa za umma.Pesa zitakazi okolewa elekeza zingine kwenye mikopo ya wanafunzi.

Mh haya mambo yafanyiwe kazi, hakuna siasa hapa na hakuna sehemu siasa imezungumzwa, hii ni uhalisia na hakuna uongo hapa, hakuna uzushi mambo yote yako wazi na raia tunayaona.

Madai 20 ya Lost Genarations: Tunataka yafuatayo kutoka Serikali ya Rais Samia yafanyiwe kazi (2024)
Top Articles
Latest Posts
Article information

Author: Geoffrey Lueilwitz

Last Updated:

Views: 6007

Rating: 5 / 5 (60 voted)

Reviews: 83% of readers found this page helpful

Author information

Name: Geoffrey Lueilwitz

Birthday: 1997-03-23

Address: 74183 Thomas Course, Port Micheal, OK 55446-1529

Phone: +13408645881558

Job: Global Representative

Hobby: Sailing, Vehicle restoration, Rowing, Ghost hunting, Scrapbooking, Rugby, Board sports

Introduction: My name is Geoffrey Lueilwitz, I am a zealous, encouraging, sparkling, enchanting, graceful, faithful, nice person who loves writing and wants to share my knowledge and understanding with you.